Friday, April 16, 2010

MCHAKATO WAKUMPATA KOCHA MPYA WA TAIFA STARS

1.) leo hii tanzania hata tupate kocha wa aina gani, ndoto za kushinda ndani ya mwaka mmoja hazipo sababu bado tunahitaji mikakati na maandalizi ya muda mrefu.

2.) angalia rekodi ya makocha maarufu na uangalie wamekaa na hizo timu kwa muda gani. wengi utakuta kachukua timu ambayo tayari ilishapikwa, yaani ilikuwa na maandalizi ya muda mrefu na kutosha. kwahiyo makocha wengi wenye majina wamekuwa wakichukua timu wakati wa mavuno.

3.) kuna hii habari ya kusema kwamba kocha lazima awe na cv ya uhakika
- hapa tatizo la kwanza ni mshahara, tanzania tuna uwezo wa kulipa makocha kama capello na wengine wa dunia ya kwanza?
- mambo yanatakiwa yaende hatua kwa hatua. mbona kocha wa uganda hana cv ya kutisha lakini angalia rekodi ya uganda invyosonga mbele.

4.) imefika wakati, tanzania pia iandae makocha wazalendo. huu mtindo wa kocha mgeni na msaidizi anatuletea mgeni, ufe. tunataka kocha ambaye yupo tayari kugawa dozi kwa makocha wa kizalendo ili mkataba ukiisha, basi makocha waliofuzu tunao kila wilaya. 



Haya ni Maoni kutoka kwa MDAU

No comments:

Post a Comment